WANAWAKE PEANENI FURSA- SENYAMULE
Mkuu wa mkoa wa Dodoma mhe. Rosemary Senyamule amewataka wanawake kutumia fursa za makongamano mbalimbali ili kubadilishana maarifa na kuinuana kiuchumi bila kujali viwango vya vipato vyao na kupeana uzoefu wa Mambo mbalimbali.
Akizungumza na wanawake katika kongamano la jukwaa la wanawake la kuwainua kiuchumi mkoa lililofanyika katika ukumbi wa Cathedral jijini Dodoma leo tarehe 27/03/2023 -Senyamule Amesema wanawake wanapaswa kushirikiana na kupeana fursa mbalimbali pale zinapojitokeza.
"Kila mtu ananafasi yake Kuna wafanyabiashara, wakulima yaani hapa tunakutana watu mbalimbali na wenye uzoefu tofauti tofauti kwaiyo Ukija maeneo Kama haya hakikisha unaondoka na kitu kipya na Cha ziada bila kujali vyeo vyenu, uwezo wenu kifedha na nyadhifa zenu mkiwa hapa endeleni kuwa kitu kimoja.
"Tunazo fursa nyingi katika mkoa wetu natamani kuwaona wanawake mabilionea wengi kutoka Dodoma wametokea baada ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kutengeneza fursa nyingi kwaiyo Kama una fursa jikonekti na wenzio Kama unayo waambie wenzako hata ukiwainua watano bado umechangia kuwainua kiuchumi",Amesema Senyamule
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Marry Bwire Ameishukuru serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa kuwapa Ushirikiano mzuri pindi wanapowahitaji kufanya kazi ya jukwaa Hilo kufanyika kwa urahisi.
"Kipekee niwashukuru Uongozi wa mkoa wa Dodoma kuanzia kwa mbunge wetu mhe.Mavunde na ofisi ya Mkoa nmeshirikiana nao Sana katika kulifanikisha hili la kongamano, muda mwingine nawapigia simu usiku lakini hawakuchoka kunipa Ushirikiano niwashukuru tena na niwaombe msinichoke katika kuendelea kujenga fursa kwa wanawake wa Dodoma",Bwire
Aidha katika kongamano Hilo mhe. Senyamule amepokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tuzo ya Pongezi kwa kuanzishwa majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi Nchini Jambo ambalo wanawake wananufaika nalo.
Comments
Post a Comment