BILIONI 17 KUJENGA MNARA WA MASHUJAA NA UKUMBI
Mkuu wa
Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewapongeza wana Dodoma kwa miaka 59
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni wiki ya maadhimisho sherehe hiyo
na kuwataka vijana kuchangamkia fursa zinazoendelea kujitokeza jijini Dodoma.
Senyamule
ameyasema hayo leo alipotembea mradi wa ujenzi wa uwanja na mnara wa mashujaa
katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba.
‘’Leo nina furaha kubwa kwa kuwa maelekezo ya Mhe Rais
wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapa jijini Dodoma tarehe 25 Julai,
2022 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa yanaendea kutekelezwa na
hii ni heshma kubwa kwetu wana Dodoma kwakuwa Mradi huu kuanza kutekelezwa kwa
vitendo. Kupitia mradi huu, tunakwenda kuweka alama nyingine muhimu
itakayopendezesha Mkoa wetu ambao ndio Makao Makuu ya Nchi yetu, pia
wanadodoma watanufaika kiuchumi na kijamii” Senyamule amefafanua
Aidha
Mhe. Senyamule amewataka wakandarasi kuhakikisha wanatekeleza ujenzi wa mradi
kwa hadhi kubwa na sifa nzuri kwa kuzingatia ubora na imara kwa miundombinu na
kuzingatia muda waliopatiwa.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Senyamule amezungumzia maandalizi ya Mkoa wake kuelekea maadhimisho
ya miaka 59 ya Muungano.
"Tunaelekea
maadhimisho ya sherehe ya Muungano tarehe 26/4/2023 na hapa Dodoma tumeanza
kuadhimisha toka tarehe 17/4/2023 ambapo tunajivunia mashujaa wetu walioweza
kuunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuleta Tanzania ambayo hii leo
tunajivunia Muungano wenye mshikamano ,usio yumba, wenye mtizamo sahihi
kwa wananchi wake wa pande zote mbili na muungano ulio imarika kila sekta kwa
Tanzania na Dunia kwa ujumla "Amesema Senyamule
Kwa
upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz amesema
fedha za ujenzi zipo tayari na zinatoka kwa wakati ambapo kiasi cha Shilingi bilioni
17 zitatumika kufanikisha ujenzi wa Mnara huo wa mashujaa pamoja na
zahanati na sehemu ya kupumzikia na kusisitiza kuwa upande wa usimamizi
wamejipanga vizuri .
Nae
Meneja wa Kanda wa SUMA JKT Meja Generali Samwel Jambo ambaye pia ndio
Mkandarasi wa Ujenzi amesema wamejipanga kutekeleza kazi hiyo kwa wakati na
ubora hadi kufikia siku maalumu.
MWISHO
Comments
Post a Comment