DODOMA KUNUFAIKA NA MRADI WA BOOST WENYE THAMANI YA BILIONI 10.6








Kiasi cha   Shilingi Billioni 10.6 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Idara ya Elimu katika kipindi cha Januari  hadi Aprili 2023  kupitia mradi wa Boost kwa Mkoa wa Dodoma. Akifungua kikao hicho leo 21/04/2023, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wasimamazi wa mradi hiyo  kusimamia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha majengo yanayo kusudiwa yanakamilika kwa wakati ili kuleta tija ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyokusudia ya wanafunzi kusoma kwenye mazingira mazuri.

Akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Elimu, Maafisa Manunuzi na Wahandisi katika ukumbi wa Jengo la Mkapa jijini Dodoma, Senyamule amesema fedha hizo zimelenga kujenga miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa shule mpya za msingi 16 zitakazogharimu kiasi cha billioni 6.1, idadi ya vyumba vya madarasa 153 kwa kiasi shilingi Milioni 3,519,000. madarasa ya mfano elimu ya awali 16  yatakayogharimu kiasi cha shilingi milioni 508,800, darasa la elimu maalumu 1 litakalogharimu Shilingi milioni 23 matundu ya vyoo 106 na nyumba za walimu 3 wa gharama ya Shilingi  milioni 285

Aidha amewataka Maafisa Manunuzi kutokuwa kikwazo katika kipindi cha  utekelezaji  wa miradi hiyo pindi utakapoanza katika kuhakikisha vifaa vinapatikana kwenye mazingira ya kazi na kuwataka kununua vifaa kwa bei ambazo ni halisi na kuzingatia ubora unaotakiwa huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia kwa ukaribu fedha hizo .

Mheshimiwa Senyamule amewataka wajumbe kuhakikisha wanafanya kazi kama timu na kutoa ripoti kwa kila hatua wanayofika ili kuwa na ufanisi na katika kutoa taarifa kwa lengo la kuwa na ufuatiliaji wa karibu ili kama kutatokea changamoto kuweza kutatua kwa haraka. 

Mhe.Senyamule amewaelekeza watendaji wote kufuatilia miradi ya nyuma na kuacha uzembe katika kusimamia kazi hizo kwa kuzingatia viwango vya ubora na kutoa rai ya kutosubiri miradi kuvuka mwaka wa fedha kwani kufanya hivyo ni kuchelewesha huduma kwa wananchi.

Vilevile, kuelekea maadhimisho ya miaka 59  ya Muungano Senyamule amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote kuhakikisha wanaendelea kusherekea kwa kuratibu makongamano na ufunguzi wa miradi  mbalimbali ili kuonyesha mshikamano na umoja uliodumu kwa takribani miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Ally Senga Gugu amesisitiza wasimamizi wa miradi hiyo  kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi  kwa  kuhakikisha mradi yote inatekelezwa kwa wakati husika na kwa ubora unaotakiwa ili kuunga juhudi za Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA