KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 59 YA MUUNGANO VIONGOZI WAKIROHO JIJINI DODOMA WAKUTANA KULIOMBEA TAIFA










 

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameshiriki maombi maalumu 

ya kuliombea Taifa la Tanzania kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano

yalioandaliwa na ofisi ya yake kwa kushirikiana na Kamati ya amani chini ya uongozi

wa Sheikh Mustapha Rajab Sheikh wa Mkoa wa Dodoma.

 

Lengo la maombi hayo ni kumuombea afya njema Rais wa Jamuhuri ya muungano

wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuombea Uchumi,  kupinga uhujumu

uchumi, kukemea ukatili wa kijinsia na Ushoga, rushwa, ukatili kwa Watoto,

Watumishi wa Serikali wa ngazi zote, Vyombo vya ulinzi na usalama, hali ya hewa,

Makao makuu ya nchi na kuombea Muungano ili uendelee kudumu pamoja na 

viongozi waasisi wa Muungano wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar ambao ni

Mwalimu Julius K. Nyerere na Abeid Amani Karume.

 

Maombi hayo yamefanyika leo tarehe 24/4/2023 walipokutana  viongozi mbalimbali

wa kiimani na serikali na kuhudhuliwa na viongozi wa Serikali miongoni mwao ni

Wakuu wa Wilaya ya Chemba, Bahi na Dodoma mjini, hafla iliyofanyika katika

ukumbi wa ‘Dear Mama’ jijini Dodoma. 

 

“Tuendelee kuombea Muungano huu wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar uwe

wamfano siyo tu Afrika bali hata duniani kote  watu waseme upo muungano nchi ya

Tanzania ambao hauyumbi uendelee kuimarika kila siku, tuombee viongozi wetu kila

siku waendelee kuongezewa hekima, maarifa, upendo na utayari wa kuendelea

kutumika kwa ajili ya Watanzania  na nchi yetu iendelee kustawi kiuchumi, kuwa na

amani na utulivu ili  kuendelea kukua katika kila sekta za kijamii. 

 

“Kadhalika  kuombea mambo ya maadili ya Vijana wetu na kutoa elimu kwa vijana

kuhusu maadili mema ya nchi yetu na kuwa mstari wa mbele kupinga mambo yasio

faa katika nchi yetu “Amesisitiza Senyamule. 

 

Naye, Katibu Tawala wa Mkoa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu amewashukuru

viongozi wakiimani kwa muutikio mzuri walio uonyesha na kuwa mstari wa mbele

katika kushirikiana kwa kila kitu ikiwa pamoja na maombi amewaasa  kuwa na umoja

endelevu na kuendeleza maombi hayo  ili mambo ya maendeleo Mwenyezi Mungu

aweze kuongeza baraka. 

Aidha, maombi hayo ya kuombea taifa na maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano

wa Tanganyika na Zanzibar yamehusisha viongozi wa madhehebu ya kikristo na waislam


 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA