GWAJIMA AZINDUA PROGRAM YA JINSIA YA INTERNATIONAL FINANCE CORPORATION {IFC}

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothh Gwajima amezindua Programu ya Jinsia ya ANAWEZA itakayowawezesha wanawake kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo Mei 31, 2023. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dkt. Gwajima amesema Programu hiyo itakayogharimu fedha za Kimarekani milioni 7.5 inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 , Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya 2050, Sera ya Maendeleo na Jinsia ya 2000 na Sera ya Jinsia ya 2016 ya Zanzibar. "Uzinduzi wa Programu ya ANAWEZA ambayo inalenga kumkomboa mwanamke kiuchumi, imekuja kwa wakati muafaka ambapo Tanzania ipo katika jitihada za kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi. Tanzania ni mojawapo ya Mataifa yanayotekeleza malengo ya Jukwaa la Kimataifa ya Kukuza usawa wa Kijinsia. Katika hili Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri...