SENYAMULE ATATUA KERO ZA WAKAZI WA MBWANGA










Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo Mei 29, 2023 amefanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Mnadani, Mtaa wa Mbwanga,Tarafa ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Dodoma na kutoa ufumbuzi wa changamoto zilizokuwa zinawakabili wakazi hao.

Awali, wakazi hao wa Mbwanga wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi cha Shilingi milioni 318.8 kwa ajili ya ujenzi waShule mpya yenye madarasa 7 ya msingi na mawili ya awali shule ambayo inaenda kutatua changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Godwin Gondwe amesema katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo wananchi wamechangia nguvu zao kwa kusafisha eneo lote la ujenzi, kujitolea huduma ya maji na kupanda miti kuzunguka eneo lote la shule hiyo.

Hata hivyo Wakazi hao wametoa kilio chao mbele ya Mkuu wa Mkoa Mhe.Rosemary Senyamule kuwa wanakabiliwa na tatizo la kubwa la Maji, Umeme,Barabara na ukosefu wa huduma ya usafiri kuelekea katikati ya jiji.

Senyamule ambae aliambatana na wataalamu wa sekta husika amewahakikishia wakazi hao kuwa huduma ya maji iko mbioni kuwakifikia kwani uchimbaji wa visima maeneo ya pembezoni unaendelea ikiwa ni mpango wa muda mfupi na mpango wa muda mrefu ni kuvuta maji kutoka Ziwa Viktoria, Mtera na bwawa la farkwa lilipo wilayani Chemba.

Akifafanua kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara mwakilishi kutoka REA amesema tatizo hilo linaenda kukamilika ndani ya wiki mbili kufuatia kukamilika kwa miundombinu wezeshi ya kuimarisha umeme katika eneo hilo.

Aidha, Senyamule amesema jamii inapaswa kufahamu kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mkoa wa Dodoma ametoa Fedha nyingi katika kutekeleza miradi ya kimkakati katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu ikiwa ni pamoja reli, barabara na

viwanja vya ndege.

Pia, Senyamule amekemea mmomonyoko wa maadili katika jamii, utoro na kusisitiza agenda endelevu ya hifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

“Rais wetu ameboresha miundombinu ya elimu, hakikisheni Watoto wote wanaenda shule, simamieni maadili na turudi kwenye jukumu la msingi la kutimiza wajibu wetu katika malezi ya Watoto.” Senyamule amesisitiza.

“Sote tukumbuke kuwa suala la mazingira ni agenda ya kudumu, kila kaya ipande miti mitano na kuitunza ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani” Senyamule ameongezea.

Mhe. Senyamule amefanya ziara ya kukagua hatua za ujenzi wa miradi ya Boost ikiwa ni pamoja na Shule mpya, madarasa ya Shule za Msingi na awali, ujenzi wa majengo ya Utawala na matundu ya Vyoo. Katika ziara zake Mhe.

Senyamule pia amepata fursa za kufanya mikutano ya hadhara kwa maeneo aliyotembelea, kusikiliza kero za wananchi wa maeneo husika na kuzitolea ufafanuzi kutoka kwa wataalamu alioambatana nao.

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA