SENYAMULE AZINDUA PROGRAM YA WANAWAKE, UCHUMI NA VIWANDA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua Programu ya zunguka na Dkt. Samia ya wanawake na Uchumi wa Viwanda (WAUVI) Mkoa wa Dodoma wenye dhamira ya kuwainua wanawake kiuchumi na kukuza thamani ya mazao mbalimbali ya kimkakati Mkoani humo kupitia Semina na Mafunzo Mbalimbali yanayoandaliwa na Uongozi wa WAUVI.
Uzinduzi huo umefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Nyerere Square jijini humo ambapo Mhe. Senyamule amewapongeza wanachama wa chama hicho na kuwataka waendelee kuhamasishana ili kuwa na wanachama wengi zaidi na kuboresha uchumi wao.
"Niwapongeze kwa kuanza na kuthubutu nimesikia mikakati yenu kuwa mlianza na wanachama 65 pekee lakini leo ikiwa ni miaka miwili pekee mmefikia wanachama zaidi 3,700 hii ni idadi kubwa sana hongereni sana na nimeskia mmepanga kuwa na wanachama 10,000 kwa kasi hii mliyokuwa nayo inawezekana endeleeni kuhamasishana.
"Maono yenu ya kuhakikisha wanachama wa WAUVI wanakuwa na nguvu ya kiuchumi nimeona pia kuna wanaume kwenye chama hiki ambao ni asilimia 20 na wanawake ni asilimia 80 na mmeshafikia Wilaya 3 za Kondoa, Chamwino na Dodoma Jiji niwaombe mfike pia katika Wilaya zote za Dodoma ikiwemo Wilaya ya Bahi kwasababu Mkuu wa Wilaya ameniahidi mkitoka hapa mtaongozana kwenda kwake", Amesema Senyamule
WAUVI ni miongoni wa Taasisi Hai isiyo ya kiserikali inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na serikali katika kufanya shughuli zake ilizinduliwa mnamo Mwaka 2021 ikiwa na wanachama 65 pekee lakini ndani ya miaka miwili imefanikiwa kuongeza idadi ya wanachama 3700 lengo kuu ni kufikisha wanachama zaidi ya 10,000.
Comments
Post a Comment