Uongozi wa shirika la Global Communities Tanzania ulifika ofisi za katibu tawala wa mkoa wa Dodoma Bw Ally Gugu kwa lengo la kuwasilisha na kutambulisha rasmi mradi wa “Pamoja Tuwalishe”.
Mradi huu kwa kushirikiana na serikali, jamii na wadau una lengo la kuimarisha lishe katika shule za awali na msingi ili kuboresha elimu katika wilaya tatu za mkoa wa Dodoma ambazo ni Chemba, Kondoa na Bahi.
Ma lengo ya mradi huo ni Kuboresha ujuzi wa wanafunzi; Kuboresha afya na Lishe ya wanafunzi;Kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa Muongozo wa chakula na Lishe shuleni.
Comments
Post a Comment