SENYAMULE ARIDHISHWA NA UJENZI MNARA WA MASHUJAA
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amekagua na kuridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Mnara wa Mashujaa unaojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kwa dhamira ya kuwaenzi Mashujaa mbalimbali waliopigania Taifa la Tanzania.
Senyamule amefanya ukaguzi huo Leo Tarehe 26/06/2023 ikiwa ni ziara ya kikazi ya Maandalizi ya siku ya Mashujaa Nchini inayotarajiwa kudhimishwa Julai 25,Mwaka huu na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais waTanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan
Comments
Post a Comment