SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI DODOMA
Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia
Suluhu Hassan
imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jiji la
Dodoma kwa lengo la
kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Ndugu
Daniel Chongolo katika viwanja vya Mtekelezo vilivyopo Shule
ya Sekondari Central
Jijini Dodoma akihitimisha ya ziara yake ya siku kumi
ndani ya Mkoa wa Dodoma.
Ndugu Chongolo amesema kuwa changamoto hizo ni pamoja na
migogoro ya ardhi,
sekta ya kilimo, elimu, Maji na ubovu wa miundombinu ya
kufika kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya. Ndugu Chongolo amesema kuwa lengo la
ziara yake
mkoani humo ni ilikuwa ni kusikiliza wananchi wa Mkoa
wa Dodoma na kutatua
changamoto zao.
Vile vile amewaasa wafanyakazi wote waliopata nafasi za
ajira kwenye miradi
mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kufanya kazi kwa bidii
ili kulinda ajira zao
pamoja na kuacha tabia ya wizi na kuchukua vitu visivyo
halali badala yake
watangulize uzalendo mbele kwa maendeleo ya Mkoa na
taifa kwa ujumla.
Naye Naibu Waziri OR-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi
amesema barabara
zinaendelea kuboreshwa na kutengewa fedha kwa ajili ya
Ujenzi na kukamilishwa
kwa Zahanati na Shule ya Sekondari. Aidha amesema kuwa
changamoto za
miundombinu ya Zahanati ya Chali iliyopo Wilaya ya Bahi,
Kituo cha afya cha
Msaada Wilayani Chemba vyote vitakamilishwa.
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. Dkt.
Angelina Mabula
amewataka wananchi wanaonunua ardhi kuanzia kwenye
Halmashauri kabla ya
kununua ili kupunguza migogoro ya ardhi na utapeli
Mheshimiwa Mabula amesema hayo wakati akijibu hoja kuhusu
migogoro ya ardhi
iliyopo ndani ya jiji la Dodoma kwani hadi sasa migogoro mingi
ya ardhi imefanyiwa
kazi na ipo kwenye ngazi za Kiutawala kwa ajili ya Uamuzi.
Amesema kuwa Wizara
yake imeweka Makamishina wawili wa ardhi maalumu, ambapo
mmoja
atashughulikia migogoro ya jiji na mwingine nje ya jiji.
Huku, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kiwanda cha
kuchakata zabibu
kitajengwa na kitaendeshwa na sekta binafsi na viwanda
vilivyopo ndani ya Mkoa wa
Dodoma ikiwa ni pamoja na kuendelea kukamilisha skimu za
umwagiliaji Mkoani
Dodoma.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary
Senyamule
amesema ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
imekukuwa na manufaa
kwakuwa ameweza kupata elimu na kujifunza vitu mbalimbali
sambamba na
kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza na kuahidi
kuendelea kutekeleza Ilani ya
Chama cha Mapinduzi kikamilifu. .
MWISHO
Comments
Post a Comment