UONGOZI WA VODACOM WAMTEMBELEA RC-SENYAMULE
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amekutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Vodacom Tanzania waliofika Ofisini kwake leo Juni 27, 2023 kwa lengo la kujitambulisha na kuimarisha uhusiano uliopo baina yao na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia katika Maendeleo ya Mkoa wa Dodoma na Taifa kwa ujumla.
Katika mazungumzo yao Kampuni ya Vodacom Tanzania Ltd imelenga pia kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa kuandaa mfumo uliounganika wa kutoa huduma hizo ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa takwimu.
Ugeni
huo umeongozwa na Bw. Philip Besiimire Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,
Bi.Zuweina Farah Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania na Bi.
Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Serikali Vodacom Tanzania.
MWISHO
Comments
Post a Comment