Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Joyce Ndalichako amempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Khadija Taya (Keisha) kwa kuandaa Chakula Cha Mchana kwaajili ya watu Wenye mahitaji Maalumu katika Mkoa wa Dodoma.

Pongezi hizo zimetolewa katika Hafla ya chakula hicho iliyofanyika leo tarehe 28/06/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Jengo la Mkapa ambapo amekiri Serikali kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha Mahusiano mazuri na Watu Wenye mahitaji Maalumu.

"Kwa hakika hili ni Jambo kubwa linaloonyesha upendo na namna ambayo unawathamini watu wenye mahitaji Maalum na kaulimbiu ya 'upendo kwa watu Wenye Ulemavu ni upendo kwa jamii nzima' hii ni kaulimbiu ambayo inatukumbusha wanajamii wote kuwakumbuka watu Wenye mahitaji Maalumu nakupongeza sana kwa Jambo hili",Amesema Ndalichako.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule amesema kati ya wakazi milioni 3 wa Mkoa huo unakadiriwa kuwa  asilimia 1 ni walemavu na Mkoa unatambua kuwa Ulemavu ni kundi Muhimu hivyo linahitaji kupata Ustawi sawa na Wananchi wote.

"Mkoa wa Dodoma tunakadiriwa kuwa na walemavu asilimia 1 ambayo ni sawa na walemavu 30,000 kwa Mujibu wa matokeo ya Sensa ya Mwaka 2022, Mkoa wetu una Halmashauri nane na tatu kati ya hizo zimeshaunda kamati ya watu Wenye Ulemavu kwa asilimia 100 na kamati 735 zimeundwa kati ya Kamati 819 zinazotakiwa kwa ngazi za mitaa na Vijiji" Amesema Senyamule

Kwa upande wake Mratibu wa hafla hiyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Khadija Taya Amesema Halmashauri zimekuwa zikitenga asilimia 30 za manunuzi ya ndani ya Serikali hivyo ametoa rai kwa wenyeulemavu kuchangamkia fursa hizo.

"Serikali imekuwa ikitenga asilimia 30 ya manunuzi ya ndani ya vifaa kwa ajili ya watu Wenye mahitaji Maalumu kwahiyo niwatoe uoga, Fedha zile ni kwaajili yenu tuchangamkieni fursa Serikali inapotangaza kwa kuunda vikundi na kufanya kazi mbalimbali ambazo mna uwezo nazo na mtakuwa mnajiongezea vipato vyenu".

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA