DODOMA YAONGOZA KWA WINGI WA MADINI YA AINA TOFAUTI
Taasisi
ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) leo tarehe 28/07/2023
wamewasilisha taarifa ya utafiti wa Madini yanayopatikana nchini Tanzania huku
Dodoma ikiongoza kwa kuwa na orodha ya madini ya aina nyingi.
Akiwasilisha
taarifa hiyo leo Meneja Jiolojia kutoka (GST) Bw. Maswi Solomon amesema kuwa
utafiti huo umeonyesha miongoni mwa madini matano ya kimkakati madini manne
yako katika Mkoa wa Dodoma.
Amesema
Mkoa wa Dodoma ni maarufu kwa upatikanaji wa miamba yenye madini ya lithium, chrysoprase, chuma, nikeli, urania na jasi. Aidha, taarifa hiyo
imeonyesha kuwa kuna madini ya yoderite
yanayopatikana Mlima wa Mautia Wilayani Kongwa na imebainika kuwa madini haya
hadi sasa yanapatikana Tanzania pekee duniani kote.
Akipokea
taarifa ya utafiti huo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema
taarifa hiyo itakuwa ni nyenzo itakayosaidia kuutangaza Mkoa wa Dodoma kimkakati husasan
katika uwekezaji wa sekta ya madini.
“Nawashukuru
sana GST kwa kuwasilisha kitabu hiki na ramani ya inayoonyesha madini katika
Mkoa wa Dodoma, ni taarifa muhimu sana ya kuvutia wawekezaji kwa kuwa
imeainisha aina ya madini na eneo yanapopatikana” Senyamule amesisitiza.
Aidha,
Senyamule pia ametoa wito kwa jamii kutumia taasisi hiyo ya Serikali katika
kufanya utafiti wa ardhi kabla ya kuanza kwa ujenzi wa ghorofa katika ya 3-4
ili kuepuka madhara.
Pia,
ametoa rai kwa taasisi hiyo kushirikiana na Bonde la Wami Ruvu katika
kuendeleza tafifi za wingi wa maji katika bonde hilo kwa kuwa taasisi ya GST
imethibitisha kuwa na vifaa na utaalamu wa kutosha.
Jiolojia
ya Mkoa wa Dodoma imegawanyika katika makundi manne huku sehemu kubwa ikiwa ni
ile ya kundi la miamba ya Archean ya Dodoman na Nyanzian ambayo baadhi yake ni maarufu kwa upatikanaji wa madini ya
dhahabu, ila kwa Dodoma miamba hii ina madini ya chuma, urani, nikeli na
lithium.
Aina
ya pili ni miamba ya Usagaran ambayo
ni maarufu kwa uwepo wa madini ya vito, chuma na shaba. Aina ya tatu ya miamba
ni ile ya ukanda wa Neoproterozoic
Mozambique Mobile Belt inayopatikana Wilaya za Kondoa, Mpwapwa na Kongwa na
maarufu kwa madini ya shaba na vito hasa ruby. Aina ya nne ni ile ya Neogene inapatikana katika maeneo ya
Farkwa na Mpondi Wilaya ya Chemba, Gonga na Kondoa.
MWISHO.
Comments
Post a Comment