JITAHIDINI KUPINGA UKATILI KWA WATOTO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu amewaasa Maafisa Afya, Lishe , Elimu, Ustawi na Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri zote 8 za Mkoa huo kutekeleza Mpango wa Taifa wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) ili kukabiliana na changamoto za ukatili kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 0-8.
Wito huo umetolewa leo Julai 28,2023 katika Kikao kazi cha kujadili namna ya kujenga uelewa na kutoa taarifa za utekelezaji za kazi zinazofanywa katika Halmashauri zote kwa robo nne ya mwaka na kujenga uelewa kuhusiana na utekelezaji wa programu hiyo iliyozinduliwa rasmi tarehe 21/09/2021 na kufikia maazimio ya utekelezaji wa majukumu waliyoazimia.
Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa Jijini Dodoma.
"Wataalamu wote mliopo hapa toka sekta zote 5, mfanye kazi kwa kushirikiana katika kutekeleza programu ya MMMAM kwakuwa mnahusika katika ulinzi na usalama wa mtoto mshirikiane ili kulinda tunu ya Taifa, Kila mmoja kuwajibika katika eneo lake kwa maslahi mapana ya Mtoto na Kuendelea kutoa elimu kwa jamii, viongozi wa dini na wa kimila juu ya kumlinda mtoto wa kike na wa kiume dhidi ya ukatili "ameeleza Gugu
Aidha, Bw. Gugu amesema Programu hiyo Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, inalenga kutatua changamoto za ukuaji na maendeleo ya watoto wenye umri wa miaka 0-8 Programu na ina maeneo matano ya utekelezaji ambayo ni Afya bora kwa mtoto na mama/mlezi , Lishe ya kutosha kuanzia ujauzito ,Malezi yenye mwitikio ,Fursa za ujifunzaji wa awali pamoja na Ulinzi na usalama kwa watoto.
Kwa Upande Wake Bw.,Sebastian Kitiku Mkurugenzi Wizara ya Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto ametaja aina za wanazokumbana nazo watoto wadogo wa chini ya Umri wa miaka 8 ikiwa ni Vipigo ,Kuchomwa na vitu vyenye ncha kali na kuungunzwa, ukatili wa ngono na ulawiti pamoja, ukatili wa Kijinsia na Ukatili wa kisaikolojia.
Katika kipindi cha miaka 2 ya MMMAM imefanikiwa kuwatibu watoto wenye utapiamlo mkali 1130 sawa na 99.7%, kuwasaidia wamama wajawazito 397,933 waliohudhuria kliniki kupewa vidonge vya madini chuma na Asidi ya Foliki ambayo inamsaidia mtoto aliyeko tumboni kuzaliwa bila matatizo.
Comments
Post a Comment