Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye amani duniani kutokana na maono na utashi wa viongozi wakuu wa nchi.
Akizungumza katika Ibaada ya shukrani na uzinduzi wa Kitabu cha Askofu Evance Chande wa Kanisa la Kalmel Assemblies of God Ipagala Dodoma leo Julai 30, 2023, Senyamule ametoa rai kwa jamii kuenzi na kudumisha amani iliyopo.
"Viongozi wetu Wakuu wanadhamira njema sana kwa ajili ya watanzania kupitia maneno na vitendo vyao, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi jasiri na mwenye upendo mkubwa, ameweza kuendeleza miradi ya kimkakati ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa na Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere" Senyamule amesisitiza.
Amesema Mkoa wa dodoma una mengi ya kujivunia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mji wa Serikali, Ujenzi wa Makao Makuu ya Mahakama na Ujenzi wa barabara za Mzunguko
Senyamule amesisitiza kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anagusa maisha ya mtu mmoja moja kwakuwa %60-70 ya watanzania ni wakulima hivyo katika sekta ya kilimo yamefanyika mapinduzi ya kilimo, elimu kuanzia elimu ya awali mpaka elimu ya juu, ujenzi na miundombinu ya Afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali.
Senyamule akizundua kitabu cha Askofu Chande Senyamule ametoa rai kwa watanzania kuwa na utaratibu wa kusoma vitabu kwakuwa maarifa pia yanapatikana katika vitabu.
Kwa upande wake Askofu Chande amesema Serikali imewekeza miundombinu ya kisasa katika sekta ya afya hivyo watanzania wana kila sababu ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi.
Askofu Dkt. Evance Chande amefanga ibaada ya shukrani ya Miaka 35 ya utumishi na uzinduzi wa Kitabu chake alichokiita "Ijue nguvu iliyomo katika kusifu na kuabudu" hususan katika zama hizi utandawazi.
Comments
Post a Comment