Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule  tarehe 28 Julai 2023 Ameshiriki kongamono la wadau  na wafanyabiashara wa NMB lililofanyika katika ukumbi wa loyal vilage Dodoma.


Akizumgumza na wafanya biashara na wadau wa NMB Bank Senyamule amesema kuwakumbuka wadau na kuongea nao ni jambo la muhimu na kuashiria kuwa mnawakumbuka na kuwajali kama iliyopo kauli yenu ya NMB karibu yako hivi ninawapongeza kwa jambo hili jema. 

Amesema wafanyabiashara wanamchango kubwa katika kukuza na kueneza kila huduma na kwa asilimia kubwa ya ulipaji kodi katika kazi na nafasi tunapaswa kuwajali na kuwaaminisha kwa Huduma bora.


“Tunategemea mazingira mazuri ya Huduma kwa wateja wenu na kuzidi kuongea ufanisi katika kazi na kuweza kupewa uwezeshwaji kwa wafanya biashara.

“Nimefurahi kukutana na wafanyabiashara hivo nitoe fursa kuzidi kuendeleza juhudi ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweka miundombinu mingi hivo tuchangamkia Fursa za wafanyabiashara kama nia na lengo ya Rais wetu kuwainua wafanya biashara.”amesisitiza Senyamule.


Naye Bw. Victor Dilunga Meneja wa NMB Benki Tawi la Mazengo amesema ukipata changamoto yoyote ya kifedha fika katika matawi yetu kwakuwa tunatambua na kujali mchango wa wadau wetu wa wafanya biashara na tunataka kuwafikia kwa u Karibu sana kwa kutoa Huduma zilizo bora kila maeneo”Amesema Dilunga.

Vile vile Bw.Alex Mgeni Afisa Biashara NMB Amesema kunahaja ya kuwarithisha na kuwafundisha biashara watu ambao wanatuzunguka ili hata kesho ukipata changamoto yoyote bado biashara yako inaaendelea kama kawaida.”Amesema Mgeni.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA