Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma kwa kushiriana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida wamejipanga vizuri katika kuhakikisha vijana na watu mbalimbali wanapata fursa ya kupata Elimu kupitia maonyesho ya Wakulima na wafugaji (Nananane).
Senyamule
ameyasema hayo leo julai 31/2023 Ofisini kwake Jengo la Mkapa alipozungumza na
waandishi wa Habari kuhusu Sherehe na Maonyesho hayo yanayotarajiwa
kuanza
Agosti mosi na kilele chake ni Agosti 8 mwaka huu katika viwanja vya Nane nane Nzuguni Jijini Dodoma.
"Katika maonyesho hayo kutakuwa na Teknolojia mbalimbali za kuongeza tija na faida katika mnyororo wa thamani, wadau watapata fursa za kubaini Teknolojia zitakazoongeza tija katika uzalishaji.
Senyamule amesema kuwa Dhamira ya maonyesho ya mwaka huu ni kuongeza hamasa ya uzalishaji wenye tija,kusambaza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi na uharibifu wa mazingira,kutoa ajira kwa vijana na kusambaza teknolojia za kisasa katika kilimo na ufugaji bora.
Katika kuendelea kukuza thamani ya mazao ya alizeti na Mtama Senyamule amesema ndani ya maonyesho hayo kutakuwa na kongamano la mazao ya Mtama, Alizeti na Siku maalumu ya uhamasishaji wa uzalishaji kuku wa kienyeji pia kutakuwa na Tamasha la mashindano ya Nyama choma kwa kutumia majiko ya asili.
Maonyesho ya Nanenane hufanyika kila mwaka ikiwa ni sherehe za Wakulima na wafugaji na huambatana na kauli mbiu mbalimbali na kwa mwaka huu 2023 kaulimbiu ni "Vijana na wanawake ni msingi Imara wa mifumo Endelevu ya chakula" na kauli mbiu ya maonyesho hayo kikanda ni "kilimo ni Biashara ni Uwekezaji".
Comments
Post a Comment