TANZANIA NI MOJA NA HAITAGAWANYIKA-RAIS SAMIA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendelea kuenzi mashujaa kwa
kudumisha amani na kusisitiza kuwa Tanzania ni moja na haitagawanyika.
Rais Dkt.Samia amebainisha hayo leo Julai 25.2023
Jijini Dodoma katika Maadhimisho siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambapo amesema
ni muhimu kuenzi mashujaa kwa kudumisha amani ,Umoja na mshikamano.
Aidha, Rais Dkt. Samia ameagiza mnara wa mashujaa
unaoendelea kujengwa katika mji wa Serikali Mtumba katika utekelezaji wa agizo
alilolitoa Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa 2022 ukamilike kwa wakati huku
akiagiza Wizara ya Fedha kutoa fedha kwa wakati.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama amesema mnara wa mashujaa
wenye zaidi ya mita 100 utajengwa huku agizo la Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan la
kujengwa mnara wa Mashujaa likitekelezwa.
Halikadhalika, Mhagama ameipongeza Serikali ya
awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya
kujengwa mnara wenye hadhi ya Makao makuu ya nchi Dodoma katika mji wa Serikali
.
Kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka Tanzania
imetenga siku maalum ya kumbukizi ya Mashujaa waliojitoa kulipigania Taifa la
Tanzania wengine hata kupoteza maisha yao na hii ni kama ishara ya kukumbuka
uzalendo , Ujasiri na ushujaa waliouonesha.
MWISHO
Comments
Post a Comment