Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) Bi. Aziza Mumba leo tarehe 28 Agosti ,2023  amemwakilisha  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu kufungua mafunzo kwa Watumishi wa Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kuhusu Mfumo Mpya wa Manunuzi NEST.

Bi Mumba ametoa wito kwa watumishi hao kuhakikisha wanashiriki kikamilifi na kusikiliza kwa makini ili kuyafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo kuelekea utekelezaji wake unaotarajiwa kuanza tarehe 01/10/2023 kupitia mfumo huo ambao utaanza kufanya kazi rasmi

Akifungua mafunzo hayo kwa Watumishi katika ukumbi wa Mkutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema lengo la kufundishwa Mfumo huo  mpya wa Manunuzi  ni mbadala wa mfumo wa TANePS uliokuwa ukitumika awali.

Amesema mfumo huo mpya umejengwa na kusimamiwa na Watanzania, umepunguza changamoto nyingi na utaondoa kazi kubwa kwa maafisa Manunuzi kwani Mchakato wa Manunuzi utaanzia kwa idara tumizi. 

Aidha, Katibu Tawala Msaidizi huyo amesema kuwa matumizi ya Mfumo huo mpya, taratibu zote za Manunuzi zitafanywa kwenye Mfumo ikiwa na maana kuanzia uandaaji wa mahitaji ya Idara, Uanzishaji wa tenda, Uthamini, Utoaji wa Tenda na Majadiliano.

Pia, Mfumo huo  Mpya umeanza kutumika tarehe 01/07/2023 na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi Serikalini (PPRA) imetoa muda wa miezi mitatu mpaka tarehe 30/09/2023 Mamlaka zote nunuzi kuanza kutumia mfumo wa NeST. 

Katika Hatua nyingine, Katibu Tawala Msaidizi huyo amesema hatua za kisheria zitachukuliwa na adhabu kali kwa mtumishi yeyote atakae kiuka utaratibu zilizowekwa.

"Kuanzia 01/10/2023 adhabu kali itatolewa kwa Afisa Masuuli wa Taasisi ambayo haitatumia Mfumo huu. Kifungu Na 104.(2)d cha sheria ya Ununuzi wa Umma kinatoa adhabu ya faini ya kiasi cha shilingi 10,000, 000/= milioni  kutoka mfukoni mwa Afisa Masuuli atayekiuka sheria hii". ameeleza Mumba

Mafunzo hayo ya Mfumo Mpya wa Manunuzi NEST yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku 5 kwa Watumishi wa Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA