Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule leo tarehe 13 Agosti 2023 amefunga sherehe ya Wiki ya Jamhyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) iliyoanza tangu tarehe 07 Agosti 2023 katika viwanja ya Nyerere Square Jijini Dodoma.

Akizungumza na wana JAI Senyamule amesema shughuli au kazi zinazofanywa na JAI ni zenye thamani ya juu kwa wananchi na zimetukuka mbele za mwenyezi Mungu.

“Kazi za JAI hazina ubaguzi wala upendeleo wa kabila, rangi, jinsia wala dini hata itikadi za siasa bali wanachoangalia ni kutoa huduma na kutarajia malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

“Kama mnavojua kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefungua milango ya ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi ikiwemo taasisi za kidini” amesema Senyamule.

Naye sheikh Ally Kanda kiongozi na Amiri wa JAI wa Mkoa wa Dodoma amesema JAI ilianziwa mwaka 2008 na lengo kuu ni kutoa huduma za kimatibabu kwa wenye uitaji, kuunganisha watu na kupatanisha ndugu waliopoteana,kushughulikia maiti zisizo na ndugu, kutoa misaada ya utu kwa wazee wasio jiweza, kutoa maihitaji kwa magereza kama mavazi, dawa na huduma zote.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajab amesema taasisi ya JAI inamiaka nane tangu ifike katika Mkoa wa Dodoma na inafanya kazi na kuhamasisha jamii katika maeneo tofauti na kukemea tabia ambazo hazimpendezi Mwenyezi Mungu na kukataza kutenda maovu miongoni mwa taasisi zilizokubaliwa na kupewa kibali katika Serikali yetu

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA