WAENDESHA BAISKELI WAWASILI DODOMA - TANZANIA






                                         

Kikundi cha waendesha baiskeli kinachojulikana kama East Africa Bicycle Tour, leo Agosti 28 kimewasili nchini Tanzania katika Mkoa wa Dodoma wakitokea Jiji la Kampala nchini Uganda wakiwa kwenye safari ya kuzunguka nchi za Afrika Mashariki.

 Waendesha baiskeli hao wapatao 22 wakiwa ni muunganiko kutoka nchi za Afrika Mashariki zikiwemo Uganda, Kenya, Burundi, Tanzania, Congo na Rwanda, wamepokelewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Coletha Kiwale ambaye amewapongeza kwa lengo la safari yao.

"Nawapongeza kwa Tour hii mnayoifanya ambayo lengo lake ni kuleta umoja kwa Afrika Mashariki pia kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kuwa na utoshelevu wa chakula, niwatakie safari njema huko mnapoelekea" Bi. Kiwale amesema

Bw. John Balongo ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo ameelezea lengo kuu la safari yao.

" Lengo kuu la safari yetu ni kutangaza mabadiliko ya hali ya hewa na utoshelevu wa chakula. Tunaangalia jinsi mabadiliko haya yanavyoathiri upatikanaji wa chakula na katika safari hii huwa tunakutana na jamii mbali mbali na kubadilishana nao mawazo juu ya upatikanaji na utunzaji wa chakula hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa pia tunatumia safari hii kutangaza umoja wa nchi za Afrika Mashariki" Amesema Bw. Balongo.

East Africa Bicycle Tour walianza safari yao Agosti Mosi mwaka huu Jijini Kampala nchini Uganda na wanatarajia kumalizia nchini Congo ambapo watatumia siku 58 kusafiri nchi zote za Afrika Mashariki.



 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA