MRADI WA BARABARA YA MACHINGA WAKABIDHIWA KWA MKANDARASI

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Machinga complex yenye urefu wa Km 0.65 kwa kiwango cha lami, umekabidhiwa kwa mkandarasi Oktoba 30, 2023. Hafla hiyo ya makabidhiano imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule akiwa ndiye mgeni rasmi kwenye viwanja vya soko la Machinga Jijini Dodoma. Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma Injinia Edward Lemelo, ametoa ufafanuzi wa namna utekelezaji wa Mradi huo utakavyofanyika. "Ujenzi wa Machinga complex umesainiwa tarehe 25 Oktoba kwa shilingi 1,034,876,565.55 na Mkandarasi Nyanza Road Works Limited wa Dodoma kwa kipindi cha siku 180. Leo hii tupo hapa kwa ajili ya kumkabidhi eneo la mradi tayari kwa kuanza kazi. Kukamilika kwa matengenezo haya, kutarahisisha uingizwaji wa bidhaa sokoni na pia kutaboresha mazingira ya soko letu. Ujenzi huu utaambatana na ujenzi wa kitako cha barabara Km 0.65, matabaka manne ya barabara yaani G7, G15, C1 na CRR, ...