Timu ya Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma iliyopewa jukumu la kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri za Kongwa na Mpwapwa imekamilisha zoezi la ukaguzi wa Miradi hiyo ikiwemo miradi ya Elimu, Afya na Nyumba za Watumishi.
Timu hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Bw. Jofrey Pima imefanikiwa kutembelea Miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia fedha kutoka Serikali Kuu, Miradi ya Sequip na Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Ikiwa Wilayani Kongwa timu hiyo imetembelea na kukagua Miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi unaogharimu Millioni 150, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya unaojengwa kupitia fedha kutoka Serikali Kuu unaogharimu Billioni 2.5, Shule Mpya ya Kata ya Sekondari Manungu iliyogharimu Millioni 544 Fedha kutoka Mradi wa Sequip pamoja na Ujenzi wa kituo cha Afya Pandambili uliogharimu Millioni 500 fedha kutoka Serikali Kuu.
Aidha timu iliendelea na ukaguzi wa Miradi katika Wilaya ya Mpwapwa ambapo wametembelea Shule ya Sekondari kimaghai inayojengwa kupitia Mradi wa Sequip imegharimu zaidi ya millioni 544, Ujenzi wa Jengo la Huduma ya mama na mtoto unaombatana na ukarabati wa majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa uliogharimu Millioni 900 ambapo Ujenzi umefikia 90%, Ujenzi wa Bweni la Shule ya Sekondari Mazae Millioni 125, Ujenzi wa nyumba ya mwalimu Nghambi millioni 95, Ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Kiboriani umegharimu zaidi ya millioni 193, Ujenzi wa zahanati ya Kingiti iliyojengwa kupitia Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri millioni 40, Ujenzi wa zahanati ya malolo millioni 50 Fedha kutoka Serikali kuu na Ujenzi wa Shule Mpya ya Kata malolo inayojengwa kupitia Fedha za Mradi wa Sequip millioni 544.
Baada ya kutembelea Miradi hiyo timu ilitoa maagizo mbalimbali ikiwemo kuwaagiza wasimamizi hao kukamilisha Miradi kwa wakati Kama maagizo yalivyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ya kukamilisha Miradi yote ifikapo Oktoba 30, mwaka huu.
Timu hiyo iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuhakikisha Miradi yote inakamilika kwa wakati na Ubora unaohitajika imewajumuisha Bw. Jofrey Pima Mwenyekiti wa timu, Alfred Simon (mjumbe), na Anthony Mbuba (Mjumbe).
Comments
Post a Comment