Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu leo Oktoba 26, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika Ofisi yake.
Ugeni huo kutoka NBC umefika Ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha na kukuza ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Benki hiyo na kujadili fursa zilizopo Mkoa wa Dodoma ikiwa ni miongoni mwa wadau muhimu wa maendeleo katika sekta ya uchumi wa Mkoa huo.
Ugeni huo umeongozwa na Uongozi wa Benki hiyo akiwemo Meneja wa Kanda Bw. Mirage Msuya ,Meneja wa Mahusiano kwa Wateja Binafsi Bi. Zawadi Kanyawana na Meneja Mahusiano Taasisi za Serikali Bw. Abdallah Pazi .
Comments
Post a Comment