WAZAZI/WALEZI WALINDENI WATOTO DHIDI YA UKATILI.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaasa wazazi na walezi kuwajengea watoto uwezo wa kujitambua na kujilinda dhidi ya ukatili wa kijinsia kufuatia hatari ya matukio ya ukatili na unyanyasaji yanayoendelea katika jamii. Ni katika viwanja vya 'Nyerere square' Jijini Dodoma ulipofanyika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia leo Novemba 30/2023. "Nitumie fursa ya kampeni hii ya siku 16 kuwakumbusha wazazi/ walezi na jamii kuwajengea watoto wetu uwezo ili waweze kujitambua na kujilinda dhidi ya matukio ya ukatili kwani watoto Wapo katika hatari zaid ya kufanyiwa vitendo vya ukatili. "Nitoe rai kwa watendaji katika ngazi mbalimbali kuhakikisha kunakuwa na mifumo ya utoaji wa msaada wa haraka pale inapobainika mtu amefanyiwa ukatili wa kijinsia ili manusura awezeshwe kupata huduma kwa haraka kuepusha athari zaidi," amesema Senyamule Aidha Senyamule ametaja maeneo ya kupeleka taarifa ikiwa mtu amefanyiwa ukatili ni Kituo cha huduma za Afya, D...