WAZAZI TUWAJIBIKE KATIKA MALEZI YA WATOTO - NDG. KINGWANDE.
Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) unaofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Mkoa wa Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Mary Chatanda, Novemba 23, 2023 umeendelea na ziara yake kwa siku ya pili ikiwa imefikia katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani humo.
Ziara ya Uongozi huo imegawanyika katika timu mbalimbali ambapo Naibu Katibu Mkuu Ndg. Riziki Kingwande amefanikiwa kutembelea mradi wa Ujenzi wa Vyumba 4 vya madarasa na Ofisi 3 katika Shule ya Msingi Mwaikisabe wenye thamani ya Shilingi 90,000,000 kituo cha Afya cha Soya kilichopo kwenye kata ya Soya ndani ya Halmashauri ya Chemba pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Kata za Soya na Kimaha amewataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao na kuwa walinzi kwani kwa Sasa maadili yameporomoka hivyo amewasihii kundokana na desturi ya kuamini watu kwa urahisi kwani Dunia imeharibika .
"Wazazi naombeni tuwajibike katika kuwalea watoto wetu kwenye msingi mzuri kwani ndio viongozi wa leo na kesho yao ambayo bado wanayo kubwa ,hatuwezi kukaa kimya hii hali ya sasa hivi ambayo watoto wetu wanaharibiwa kwa kukatishwa ndoto zao na kuharibiwa miili yao, utasikia huko mara mtoto amelawitiwa mara kabakwa hizi tabia tuzikomeshe " Amesisitiza Ndg. Kingwande
Vilevile, Ndg. Kingwande amezipatia ufumbuzi kero hizo ikiwemo ahadi ya muda mrefu ya gari ya kubebea wagonjwa kwenye kituo cha afya Soya na nyingine ameielekeza Halmashauri ya Chemba kuwafanikishia wananchi wake likiwemo suala la TASAF, Barabara, ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa 4 katika Shule ya Chang'ombe pamoja na mengine ambayo yatapatiwa ufumbuzi .
Comments
Post a Comment