RAIS SAMIA AMEOKOA MAISHA YA WATOTO NJITI-NDG CHATANDA
Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda,
amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan,
ameokoa maisha ya watoto njiti kwa kuongeza wodi ya Mama na Mtoto kwenye
Hospitali ya Wilaya ya Bahi.
Ameyasema hayo leo 24 Novemba 2023 katika ziara
yake ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na wanachi Katika Halmashauri ya
Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.
“Hatuna budi kumshukuru Rais wetu Mama Samia kwa
kuleta wodi yingi za Mama na Mtoto na kuokoa maisha na vifo vya watoto njiti
kwani maisha yao yalikuwa hatarini.
“ lakini tunaona wananchi wanavyofurahia huduma
zinazoletwa kwao kwani ni bora na sahihi kwa watoto” Amesema Chatanda.
Pia Chatanda, amefanya ziara ya kukagua miradi
inayotekelezwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Nyumba ya Katibu wa
UWT WIlaya ya Bahi yenye thamani ya Shilingi 7,900,000 Hospitali ya Wilaya
yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.2, na Shule Mpya ya Sekondari ya Chali
yenye thamani ya shilingi Bilioni 544 na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua
Vilevile, kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi
Mhe. Godwin Gondwe, amesema makusanyo ya ndani katika Halmashauri yake
yamefikia zaidi ya Bilioni 1.3 na kwa ujumla ambapo bajeti ambayo mpaka sasa
Halmashauri imepokea fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha shilingi Bilioni 29.
“Mapato yameongezwa kwa kipindi hiki cha Uongozi
wa Dkt. Samia Suluhu Hassan hadi kufikia asilimia 54 na yanasaidia shughuli za
Wilaya ya Bahi huku asilimia 20 zikisaidia maendeleo na asilimia 80 zikitumika
kwa matumizi mengine ya kawaida ya Halmashauri” Amesema Gondwe.
MWISHO
Comments
Post a Comment