MAAFISA ELIMU KATA WANOLEWA KUPANDISHA UFAULU.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaelekeza Maafisa Elimu Kata wa Halmashauri zote 8 za Mkoa huo kuhakikisha wanatekeleza mpango Mkakati wa Elimu wa Mkoa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024.
Maelekezo hayo yametolewa tarehe 14/12/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Msingi St. Gaspal Miyuji Jijini Dodoma ulipofanyika Mkutano kazi.
Mkutano huo uliwajumuisha Maafisa Elimu Kata wote wa Mkoa wa Dodoma kwa dhumuni la kuinua ubora wa Elimu na Ufaulu wa Mkoa wa Dodoma.
"Nawaagiza muende mkatekeleze mpango Mkakati wa Mkoa na ifikapo mwisho wa mwaka 2024 Mkoa uwe na Ufaulu ubora kulingana na malengo yaliyowekwa kwenye mpango Mkakati wa Elimu wa Mkoa kwa mwaka 2024".Ameelekeza Mhe.Senyamule
Pia ,Mkuu wa Mkoa huyo amewaagiza Maafisa Elimu hao kuhakikisha Kila Mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa muda uliopangwa kwa kushirikiana na watendaji wengine wa ngazi ya Kijiji na kata.
"Hali ya uripoti wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 haikufikia 100% kwasababu waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza ilikuwa 47,853 na walioripoti ni 43,693 sawa na 91.32% na wasioripoti ni 8.69% hivyo kwa kushirikiana na watendaji wengine wa ngazi ya Kijiji na kata kahakikisheni watoto wote wanaripoti shuleni mapema", ameelekeza mhe. Senyamule
Aidha ,Akizungumza na Makutano Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo amewaagiza Maafisa Elimu hao kuandaa na kukabidhi Maazimio Yao ya Mwaka 2024 kwa maafisa Elimu wa Wilaya ifikapo januari 5/2024.
" Nawaomba mkaandae Maazimio yenu na muyawasilishe kwa maafisa Elimu wa Wilaya kabla tarehe 5/ mwakani, lakini na nyie mtatakiwa kuwasimamia Walimu wawakabidhi Maazimio Yao kabla ya tar.5 januari , kitu cha kuwakumbusha ni kwamba januari 8 ni siku ya kuanza masomo na sio siku ya kuandaa Maazimio na Kama Mwl atashindwa kuandaa Maazimio itahesabika Afisa Elimu kata umeshindwa kazi yako na utachukuliwa hatua stahiki," Mwl. Kayombo.
Hata hivyo, Mwl.Kayombo amewaagiza Maafisa Elimu hao kuhakikisha wanatumia lugha ya kingereza pindi wanapofanya vikao mbalimbali vya kielimu na wanapokua katika mazingira ya Shule zote za Sekondari.
Kikao kazi hicho ni muendelezo wa vikao kazi vinavyofanyika ikiwa ni katika kuendelea na kuhakikisha Mkoa wa Dodoma unapanda katika Ufaulu wa Elimu ngazi ya Msingi na Sekondari kwa mwaka wa masomo 2024.
Comments
Post a Comment