"WAHITIMU TUMIENI ELIMU ZENU KUONGEZA TIJA SERIKALINI " RC SENYAMULE .
Serikali imeahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)Tawi la Dodoma katika kutatua changamoto mbalimbali kwa kuwa na wafanyakazi wenye ujuzi na weledi wa kutosha kuhudumia Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyofanyika Disemba 16,2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa St.Gaspar Jijini Dodoma.
"Serikali inaahidi kuendelea Kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Fedha katika kutatua changamoto mbalimbali, lengo ni kuhakikisha kuwa chuo kinakuwa kwanza wafanyakazi wakutosha wenye ujuzi na weledi kutosha kuhudumia Watanzania pili kuwa na miundombinu ya kutosha kuendelea kuhudumia Wanafunzi waliojiunga katika chuo hicho na pia chuo kuendeleza majukumu yake kwa ufanisi".
Aidha ,Mhe.Senyamule amewataka wahitimu na Chuo kwa ujumla kujitathmini juu ya elimu iliyotolewa na waliyoipata kuona ni namna gani inatumika kuongeza tija Serikalini na hata katika soko la Dunia hasa katika Zama hizi za Utandawazi.
Kwa upande wake ,Mkuu wa chuo hicho cha Usimamizi wa Fedha Prof .Josephat Loto ameainisha changamoto zinazozikabili chuo hicho ikiwemo ukosefo wa mabweni, uhababa wa watendakazi na gharama za kupangisha na kuomba Serikali katika utatuzi wa hayo.
Prof. Loto ameongeza kuwa chuo hicho kimefanya ushirikiano na vyuo vya Kimataifa 12 ili kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa.
"Pia Mgeni Rasmi Chuo chetu tunafanya Mashirikiano na Vyuo vya Kimataifa 12 Nchi mbalimbali ikiwemo Ulaya, Asia na Afrika ya Kusini ikiwa lengo ni kuwapa wahitimu vionjo vya Kimataifa"
Naye ,Mwenyekiti wa Baraza la chuo Prof. Emmanuel Mjema ameiomba Serikali kusaidia katika eneo la ujenzi ili waweze kujenga majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo na makao makuu ya Chama na Serikali.
"Tunaomba msaada wa Serikali ili tujenge majengo makubwa na mazuri yanayoendana na hadhi ya Chuo cha IFM na makao makuu ya Chama na Serikali katika eneo letu kubwa lililopo eneo la Nala".
Haya ni Mahafali ya 49 ya Chuo cha IFM yaliyojumuisha wahitimu 121 wanawake wakiwa 60 na wanaume wakiwa 61, ambapo Astashahada wahitimu ni 55, Stashada wahitimu 23 na Shahada ya Uzamili ni wahitimu 43.
Comments
Post a Comment