MKOA WA DODOMA WAADHIMISHA KIPEKEE SIKU YA KUZALIWA KWA RAIS MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN









Mkoa wa Dodoma ukiongozwa na Mhe. Rosemary Senyamule leo Januari 27/2024 umeadhimisha  kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutembelea kituo cha Taifa cha watoto wenye mahitaji maalum cha Samia Suluhu Hassan kilichopo kikombo Jijini Dodoma.

Akihutubia Makutano waliojitokeza katika kuadhimisha siku hiyo Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma unayo mambo mbalimbali ya kujivunia yaliyofanywa na Rais huyo ikiwemo kujengwa Miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo.

"Mhe. Rais amebeba majukumu ya pande zote Kama kiongozi, mama na raia namba moja wa Tanzania, leo sisi wanadodoma tunayo Miradi mbalimbali tunayojivunia iliyotokana na utashi na kutupatia Fedha za kutekeleza Miradi hiyo ya maendeleo ambayo inawagusa wananchi moja kwa moja, wanadodoma tunamuombea kheri katika uongozi wake," amesema Senyamule

Hata hivyo Mhe. Senyamule amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kutenda haki, kuweka vipaumbele kwa Mambo yanayogusa jamii, kuwa mstahimilivu pamoja na kuhakikisha Watanzania wanakua na Amani na furaha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, mhe Jabir Shekimweli amesema kituo hicho cha taifa kinaweza kuwa sehemu ya kuibua vipaji vya michezo miongoni mwa vijana mbalimbali wanaoishi katika mazingira hayo ndani na nje kwani wanayo miundombinu wezeshi na rafiki katika kuchagiza vipaji vipya vya michezo.

Awali Mhe.Senyamule akifuatana na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu na viongozi mbalimbali wa ngazi ya Wizara ya maendeleo ya jamii, viongozi wa Wilaya na wadau mbalimbali wa maendeleo ya jamii wameshiriki  zoezi la upandaji Miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA