WANANCHI WA DODOMA WAHIMIZWA KUTUNZA MISITU












 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Mkoa wa huo hasa wakazi wa Kata ya Zanka Wilayani Bahi kuachana na biashara ya kuuza mkaa na badala yake waanze kujishughulisha na shughuli mbadala  zitakazowaletea kipato ili kutunza misitu wa Hifadhi ya Chenene.

Wito huo umetolewa Leo Januari 25,2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero zao , Ziara hiyo imeenda sambamba na ukaguzi  wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.

 Miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa kwa kila shule katika shule ya msingi Ibihwa na Mundemu na  matundu 21 shule ya msingi Zanka yenye thamani ya  Shilingi 168,389,815.02.

"Nitoe wito wangu kwa wananchi, jaribuni kutafuta shughuli mbadala za kupata kipato cha kukuza uchumi wenu
na  kuendelea kutunza mazingira kwani kuna fursa ya Barabara ya Dodoma- Manyara. Tumieni nafasi hii kuji vipato vyetu." Amesisitiza  Mhe. Senyamule 

Aidha, amewataka  wananchi hao kutoa ushirikiano pale wanapotakiwa kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa sababu hakuna Serikali yenye nia  mbaya kwa wananchi wake hivyo waendelee kushiriki kwenye mikutano ya maendeleo inayoitishwa na viongozi wao kwenye ngazi zote za uongozi

Naye, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe.Gérald Mongela amesisitiza suala la utoro shuleni  ambapo amewataka wazazi na walezi  Wilayani humo kuwa mstari wa mbele katika kutimiza ndoto za watoto wao.

Vile vile, Mhe.Mongela amewahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari katika msimu huu wa mvua kubwa za El-nino hasa waliopo kwenye maeneo hatarishi  ya mikondo ya maji kuhama haraka kwenye maeneo hayo ili kuokoa athari zinazoweza kujitokeza.

Wananchi hao pia wamepatiwa elimu ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindi kwa kuzingatia kanuni za usafi pamoja na kuchemsha maji ya kunywa na matumizi ya vyoo.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA