Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi wa Barabara imefanyika katika Wilaya nne za Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ,ambapo kwa nyakati tofauti ametembelea Wilaya za Kongwa, Mpwapwa ,Chamwino na Dodoma jiji kujionea hali halisi ya miundombinu ya Barabara katika Wilaya hizo.


Ziara hiyo ya Ukaguzi imefanyika ndani ya siku mbili ambapo leo Januari 20 /2024 amehitimisha ndani ya Mkoa huo.

Amekagua na kujionea namna wakala wa Barabara Mkoa wa Dodoma (TANROADS) wakiendelea kutatua changamoto ya Maji ya mvua kukata mawasiliano kwa muda pindi mvua zinaponyesha katika kata ya Mtanana Kongwa, Ujenzi wa Barabara wa Km 7.5 Wilayani Mpwapwa na kujionea namna daraja la nzari linavyokwamisha shughuli za maendeleo wananchi hususani katika kipindi cha mvua na Barabara ya mzunguko Kutoka mtumba hadi veyula jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayofanya ya uwekezaji katika sekta ya miundombinu katika kuhakikisha Jiji la Dodoma linakuwa na hadhi yake ya makao makuu ya serikali.

" Nitoe shukurani kwa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya uwekezaji katika sekta ya miundombinu katika Mkoa huu wa kimkakati nimwahidi tutaendelea kusimamia kwa uadilifu na tutazitunza na tutaendelea kutunza mazingira yanayozunguka barabara zetu ili mji uendelee kuwa nadhifu na mazingira yatakuwa yametunzwa," Mhe. Senyamule

Aidha mhe. Senyamule amemhakikishi Waziri Bashungwa ushirikiano mkubwa katika kuendelea na usimamizi wa miradi hiyo ya miundombinu ili kukamilika kwa wakati na ufanisi uliopangwa na unaotakiwa.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA