CHAMWINO DC YATAKIWA KUJITAFAKARI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kukamilisha ujenzi wa uzio wa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kabla ya tarehe 30/3 / mwaka huu.
Maagizo hayo yametolewa Leo Februari 21,2024 baada ya kuonekana kudorola Kwa mradi huo Kwa zaidi ya miezi 8 tangu ulipotakiwa kukamilika mwezi julai 2023.
"picha ya Chamwino Kwa Sasa siyo nzuri, Mkoa una Halmashauri nane na katika Halmashauri hii kila miradi inayokuja lazima zijitokeze changamoto, tunapokea malalamiko yenu mengi hasa suala la malipo Kwa wakandarasi wanaojenga miradi yenu, Mhe.Rais anatoa fedha zote ila nyie mnachelewesha kuwalipa na hiyo ndio sababu inachangia mradi kutokukamilika kwa wakati. nitoe maagizo tarehe 30/03/2024 mradi uwe umekamilika kwa ubora wake na ukamilike kwa fedha ambazo zilitolewa na ikiwezekana fedha zibaki na zifanye kazi nyingine". Ameelekeza Mhe.Senyamule
Aidha Mhe. Senyamule amemsimamisha kazi mtendaji wa kata ya Manchali Bw.Waitara Wambura Kwa kuonesha utovu wa nidhamu na kukiuka maadili ya kazi kutokana kulewa pombe katika masaa ya muda wa kazi na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kufanya uchunguzi wa kina juu ya utendaji kazi wa mtendaji huyo.
Kwa upande wake kaimu Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe. Godwin Gondwe ameahidi kusimamia bega Kwa bega miradi inayotekelezwa katika wilaya hiyo na kukamilika Kwa ubora na muda uliopangwa.
Mhe.Senyamule ikiwa ni muendelezo wa xiara zake za kikazi amekagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa ,Ujenzi wa uzio wa Jengo la ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino, Ujenzi wa Zahanati ya Wilunze ,eneo la maadhimisho ya siku ya wanawake pamoja na kufanya Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Manchali
Comments
Post a Comment