RC SENYAMULE KUDILI NA WATAKA RUSHWA





Suala la kuongea, kusikiliza na kutatua kero  za makundi mbalimbali ya wakazi wa Jiji la Dodoma wakiwemo wafanyabiashara, madereva boda boda, wachimba madini n.k limekua endelevu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na lenye matokeo chanya na muitikio mkubwa kwa makundi husika.

Februari 11/2024 katika ukumbi wa New Generation- Kisasa  katika semina ya siku moja ni zamu ya Mafundi Ujenzi wa Mkoa wa Dodoma ambao nao wanapata wasaa wa kuteta na Mhe. Senyamule ambae anawahakikishia kupambana na wote wanaoleta vikwazo mbalimbali ikiwemo kuombwa rushwa pindi wanapoomba kujenga Miradi ya Serikali pale inapotangazwa licha ya kukidhi vigezo muhimu.

"Naomba niwahakikishie kuwa tunaendelea kushughulika na wote wasio na dhamira njema na Mhe. Rais ya kutamani nyie mfanye kazi za Ujenzi wa Miradi ya Serikali bila kikwazo pale mnapokidhi vigezo, namba zetu mnazo mkikutana na vikwazo vya rushwa wakati mnaomba kazi tutumieni meseji na sisi tutashughulika nalo kwa haraka sana", ameahidi Senyamule

Hata hivyo kumekua na baadhi ya Mafundi wasio waaminifu wanaoshindwa kuwalipa Mafundi wasaidizi kwa wakati licha ya wao kulipwa na Serikali Stahiki zao, Mhe. Senyamule amebaini tatizo Hilo na kuwataka Mafundi kuwa na utu na kuzingatia makubaliano waliyojiwekea ili kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa.

"Wapo Mafundi ambao hawawalipi vibarua wao kwa wakati na hiyo ni changamoto tumekutana nayo katika baadhi ya maeneo, licha ya kwamba wao wameshapokea Fedha kutoka serikalini sasa Kama mnavojua mtu asipolipwa stahiki zake anakua na ugumu na kazi zinakua zinafanyika kwa kusua sua sasa walipeni wenzenu ili kazi zifanyike kwa haraka na ufanisi mkubwa Kama ulivyotarajiwa", amesema Senyamule.

Aidha  Mhe. Senyamule ametoa wito kwa mafundi ambao hawajajiunga na Chama Cha mafundi rangi na Ujenzi (CHAMARAUTA) kujiunga na chama hicho kwani Kuna tija kubwa ya kuwa na chama hicho hususani katika kujipatia kazi na vitu vingine vya msingi katika kazi yao

Akizungumza kwa niaba ya wengine Mkurugenzi wa RockMax international Limited Hamoud Abdallah amesema  takribani  mafundi 1,000 wa Mkoa wa Dodoma  walioajiriwa na waliojiajiri ikiwemo mafundi wa Serikali na kutoka sekta mbalimbali wamehudhuria semina hiyo.

"Mafundi waliohudhuria hapa ni takribani mafundi 1000 na hii ni matumaini ya kwamba wataenda kuwa mabalozi wazuri na kufundisha wengine huko katika maeneo yao
 ya Kazi", amesema Abdalla 

RockMax International Limited ambao ni watengenezaji wa bidhaa mbalimbali za Ujenzi hususani extra power skimming putty ndio walioendesha semina hiyo ya siku moja , Februari 11,2024 kwa mafundi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA