SENYAMULE AKEMEA UHARIBIFU WA MLIMA SAUNA-KONDOA
Ikiwa ni muendelezo wa ziara za kikazi za Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kukagua na kuhamasisha utunzaji endelevu wa mazingira kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amefika Wilayani Kondoa kujionea namna shughuli mbalimbali zinavotekelezwa Wilayani humo.
Akiwa Wilayani humo amewataka wananchi wa Kata ya Bereko hususani Kijiji cha Kisese wanaofanya shughuli za kilimo katika mlima Sauna kupanda miti katika mashamba yao na kuachana na shughuli za kilimo na uchimbaji wa madini Ujenzi katika mlima huo.
Senyamule ametoa maagizo hayo Februari 9/2023 alipofika kujionea namna ambavyo mlima huo umeathiriwa na shughuli za mbalimbali za kibinadamu.
"Suala la kutunza mlima huu tulipe uzito na tusilete lelemama, viongozi wa hapa hakikisheni kila mtu anayelima katika eneo hili anapanda Miti kwenye shamba lake ndani ya wiki mbili ikiwa ni ishara kuwa mwaka huu ni wa mwisho kulima hapa na hatolima tena.
Aidha Mhe. Senyamule amewasihi wananchi wa Kata hiyo kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi ikiwemo kuwaainisha wote wanaojihusisha na masuala hayo katika hifadhi ya mlima huo.
"Kuna Siri muhimu za kuficha na Kuna nyingine ukizificha unapoteza uzalendo wako, hizi Siri mnazofichiana wanakisese hazitakiwi kufichwa kwasababu mnawaficha watu wanaoharibu mlima ambao unapoendelea kuharibiwa uasili wake unaweza kuleta madhara makubwa, niwasihi Kila mmoja awe kiongozi na mlinzi wa mwenzie ili mlinde mazingira yenu", amesema Senyamule.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amesisitiza kuwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule yanapaswa kufuatwa na kwamba serikali ya Kijiji imeondolewa kwenye usimamizi wa msitu huo.
Naye Kaimu Muhifadhi wa Misitu Wilaya ya Kondoa Bw. Amon Mgimwa amesema watasimamia sheria za Misitu na mazingira kulinda uoto wa eneo Hilo ikiwa ni pamoja na kufanya doria ya kuwasaka waharihifu na kuwachulia hatua Kali kwa mujibu wa sheria.
Comments
Post a Comment