SENYAMULE APOKEA MAUA YA UPENDO KWA NIABA YA RAIS







 Ikiwa ni siku ya wapendanao Duniani ambayo huadhimishwa  Kila mwaka Februari 14, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amepokea maua ya upendo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Zawadi hizo zimetolewa na Wadau mbalimbali ambao Wametoka katika Mikoa ya Arusha,mara na Zanzibar huku wakiongozwa na kampeni ya "MAUA YA MAMA".

Kikundi hicho kimehusisha  waendesha baiskeli na na boda boda  ambao walianza safari Yao katika Mkoa wa Mara na leo hii wamehitimisha safari Yao katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.


#upendokwamama
#mauayamamasamia
#Dodomafahariyawatanzania
#Happyvalentineday

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA