Shirika la Global Communities Tanzania kupitia mradi wa ‘Pamoja Tuwalishe’ unaotekelezwa katika shule 75 za Msingi  kwenye Halmashauri tatu za Mkoa wa Dodoma ambazo ni Mpwapwa, Kondoa na Chemba, wamekabidhi vishikwambi 75 kwa uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kukusanya taarifa na kupata mafunzo mbalimbali ya lishe kwa njia ya kidigitali kwa shule 75 zitakazopatiwa Vifaa hivyo.

Pia Mradi huo unatoa ufadhili wa Chakula ( Mchele, Maharage na mafuta ya kupikia ) kwa shule  hizo huku dhamira kuu ikiwa kusaidia kuboresha juhudi za kusoma na kupandisha ufaulu kwa wanafunzi pamoja na kuimarisha afya na lishe bora kwa wanafunzi.  

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Februari 09, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuuwa Mkoa Jengo la Mkapa ambapo waliokabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Global Communities Tanzania ni Kaimu Mkurugenzi Bi. Vicky Macha, Meneja Mwandamizi wa Ufuatiliaji, tathmini na mafunzo Bw. Wilfred Donath na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bw. Heri Mcharo na vimepokelewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma  Bi. Coletha Kiwale.

Hata hivyo Shirika la Global Community Tanzania linafanya kazi zake kwa ufadhili wa kitengo cha kilimo cha Marekani (USDA).


 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA