TATHMINI KUFANYIKA BONDE LA MZAKWE, WAKAZI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO

 Wananchi wanaoishi  maeneo ya karibu na Bonde la Mzakwe wametakiwa kutoa ushirikiano katika zoezi la tathmini linalofanyika na timu ya watalaam ambayo imeundwa kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za  maeneo hayo ili kusadia  ushauri na  maamuzi  yatakayotolewa  katika harakati za kunusuru bonde hilo ambalo ndio chanzo kikuu cha Maji kwa Mkoa wa Dodoma.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa  Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule Februari13,2024 wakati akiitambulisha timu hiyo  kwa wananchi wanaoishi maeneo ya Bonde hilo na  maeneo jilani ambapo utambulishi huo umefanyika katika  Ukumbi wa Veyula Jijini Dodoma.

"  Kuna timu ya watalaam itapita kwenu kuja kupata taarifa ni watu wanaokuja kwa amani na wakute amani ,watafanyakazi kwenye maeneo yanayozunguka Bonde watapita nyumba kwa nyumba Ili kupata taarifa za Msingi na hiyo kazi kuanzia tarehe 14 hadi  21 Februari ", Amesema Senyamule 

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri amewaomba na kuwaagiza wenyeviti wa Mitaa na Vijiji ambao tathmini hiyo itafanyika katika maeneo yao, kuwatumia wazee maarufu na wazaliwa wa wa maeneo yao ili wawasaidie kukusanya taarifa zisizo na mkanganyiko na zenye maslahi katika tathmini hiyo ambayo Ina lengo la kulinusuru bonde hilo.

Naye Mkazi wa Kijiji cha Mundemu akizungumza kwa niaba ya wakazi wanaolizunguka bonde hilo Bw.Ayub Chimuli  amemshukuru Mhe.Senyamule kwa kuja na mchakato huo wa kupatia ufumbuzi wa eneo hilo la Bonde kwani  imekuwa ni changamoto ya muda mrefu kwa wakazi hao.

Timu ya Tathmini hiyo imeundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  kutokana na uwepo wa shughuli za kibinadamu ikiwemo kuchunga mifugo ndani ya hifadhi, kilimo na ukataji Miti ambazo zinaathiri upatikanaji wa Maji Mkoani humo.

Tathmini hiyo itafanywa na wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Maji, Bonde la wami ruvu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,DUWASA,  Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na wadau mbalimbali wa Maji na mazingira.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA