WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA MAJARIBIO YA UFUNDISHAJI MUBASHARA
Wazari wa Nchi ,Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Mohamed Mchengerwa Leo Februari 7,2024 amezindua majaribio ya ufundishaji mubashara (Live Teaching) katika Shule ya Sekondari ya Dodoma .
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mkoa na Wakurugenzi wa Halmashauri Nchini kuhakikisha wanateua Shule moja kwa kila Mkoa zitakazotumika kusambaza mfumo huo kwenye maeneo yao
"Wakuu wa mikoa pamoja na makatibu tawala wa mikoa wahakikishe kwamba wanateua Shule maalum ambazo zitakuwa nguzo ya kusambaza mifumo hii ya TEHAMA katika Shule mbalimbali kwenye maeneo yao"
Amesema Waziri Mchengerwa
Uzinduo huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule, Wakuu wa Wilaya na Maafisa elimu
Comments
Post a Comment