MHE. SENYAMULE AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA BIASHARA MKOA











Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule  tarehe 24.05.2024 ameongoza kikao cha baraza la biashara la Mkoa huo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Jengo la Mkapa.


Lengo la kikao hicho ni kujadili masuala la biashara na uwekezaji kikiongozwa na mada mbalimbali ambazo ni  pamoja  na mfumo wa masoko wa kieletroniki, matokeo ya tathmini ya mazingira ya biashara yanayokwamisha ukuaji wa biashara kwa sekta binafsi na wasilisho kuhusu stakabadhi ghalani .

Sambamba na hayo kikao hicho kimeazimia mambo kadhaa ikiwamo timu ya watalaam iundwe kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo  Mkoa huo na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuboresha namna  kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo (machinga) nk.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya amewahimiza wadau wa sekta binafsi na Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya uwekezaji katika sekta ya  maliasili na utalii hususani ufugaji wa  nyuki kwani ni ufugaji  wa  muda mfupi na ambao utasaidia kukuza uchumi wa kukidhi mahitaji muhimu.

Awali Afisa Kilimo Mkoa huo Bw.Bernard Abrahamu  ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla  kuchangamkia fursa ya maonesho ya nanenane ambayo  kitaifa yanafanyika Jijini hupo.

Ameongeza kuwa zipo fursa mbalimbali  ambazo ni pamoja na upatikanaji wa huduma zote sehemu moja (one stop center) zikiwemo bima na kwamba maonesho hayo yatakuwa ya muda wa siku nane kuanzia tarehe 01/08 - 08/08/2024 na kuwakaribisha wafanya biashara kutumia  maonesho hayo kwani yanahusisha kilimo kwa mapana na wananchi wanahamasishwa kupelaka bidhaa zao kwani ni eneo la biashara.

&&&

#keroyakowajibuwangu
#dodomafahariyawatanzania

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

‘WANAWAKE NA SAMIA’ 3000 MKOA WA DODOMA KUPATA MAFUNZO VETA