TAWEN YAZINDULIWA DODOMA










 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Mei 25, ameshiriki uzinduzi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kama Tanzania Women Empowerment Network (TAWEN) Mkoani humo  ambapo mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo kwenye ukumbi wa mikutano jengo la PSSF .

Taasisi ya TAWEN inawasaidia na kuwawezesha wanawake na wasichana kutambua mchango wao na kuthibitisha misingi sawa ya kiuchumi, kiuongozi na kitamaduni katika kutengeneza jamii yenye usawa kimawazo na kimaendeleo.

Hatahivyo huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi hiyo ni pamoja na kutoa taarifa za kibiashara, uandaaji wa makongamano na maonesho, kuwajengea uwezo wanawake kupitia mafunzo mbalimbali, kutoa ushauri wa kibiashara, kufanya utetezi na ushawishi kwa niaba ya wanawake katika masuala ya sera na Sheria mbalimbali na kuwasaidia wanawake kupata masoko yenye uhakika wa bidhaa zao.

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA