WAKAZI WA MTERA WAIOMBA SERIKALI KUSHUGHULIKIA ADHA YA MAMBA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewasihi wakazi wa Kijiji cha Mtera kuwa wavumilivu wakati mchakato wa Serikali unaendelea kuhusu zoezi la uvunaji wa Mamba katika bwawa la Mtera kutokana na wanyama hao kusababisha vifo mara kwa mara kwa wakazi wa eneo hilo.
Mhe. Senyamule ametoa wito huo Mei 29, 2024 kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mtera na kuibua kero hiyo ya Mamba na kuomba Serikali iendeshe zoezi la uvunaji wa mamba hao katika kijiji hicho.
Kwa Upande Wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya amewaelekeza watendaji wa vijiji kuwa wawazi kwa wananchi wao inapotokea Serikali inatekeleza Jambo la maendeleo kwa wananchi kwa kutoa taarifa kwenye mikutano ya hadhara na kubandika matangazo sehemu mbalimbali.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya amewasihi wakazi wa Mtera kukaa mbali na vitendo viovu kwa kutii Sheria bila shuruti ili kujiepisha na Mkono wa Sheria.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment