DODOMA YANG'ARA RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI












 Mkoa wa Dodoma umefanikiwa kupata hati safi katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu zilizoishia Juni 30,2023.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Juni 19, 2024  Wilayani Chamwino Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezipongeza Halmashauri zote za Mkoa huo kwa juhudi zake katika kupunguza hoja za Mkaguzi na kupata hati safi.

" Sasa hivi Mkoa wa Dodoma wote umepata hati safi ,tunategemea sasa ni mwendo wa hati safi kwa Halmashauri zote. kazi yetu kubwa ni kuendelea kupunguza zile hoja ndogo ndogo za Mkaguzi ili nazo ikiwezekana kama siyo kumaliza basi zipungue kwa kiwango kikubwa" Ameeleza Mhe. Senyamule 

Kwa upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja amewasihi Menejimenti ya Wilaya hiyo kumtumia vizuri mkaguzi wa ndani kila anapotoa taarifa za kila  robo ya Mwaka wa fedha ili kupunguza hoja kwa Mkaguzi Mkuu.

Kadhalika Mhe.Senyamule, Katibu Tawala Mkoa Bw.Kaspar Mmuya kwakuambatana na Uongozi wa Wilaya hiyo kutekeleza kauli mbiu ya " kero yako wajibu wangu" kwa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Msanga kilichopo Wilayani humo.

&&& 

#keroyakowajibuwangu 
#dodomafahariyawatanzia

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA