"UTUNZAJI MAZINGIRA NI SUALA LA KIIMANI KWANI NI AGIZO LA MUNGU" RC SENYAMULE




 Wito umetolewa kwa waumini wa Madhehebu mbalimbali, kuzingatia utunzaji wa Mazingira kwa kutumia nishati Safi kwani ni moja kati ya maagizo ya Mungu. Hayo yamesemwa wakati wa kufunga Kongamano la Maombi ya toba ya urejesho wa thamani ya Afrika 2024.

Kongamano hilo kubwa lililofanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Mwangata uliopo Barabara ya Singida Jijini Dodoma, limefungwa June 28, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na lilishirikisha wanamaombi na wachungaji kutoka nchi tano za Afika.

"Mazingira ni Imani kwani Mungu ametuagiza tutunze Mazingira. Tuungane katika matumizi ya nishati Safi ili kulinda mazingira yetu yanayoweza kuathiri Dunia nzima. Kupitia Maombi haya, naona mabadiliko kwa Dodoma na Afrika kwa ujumla kwani suala hili limewakutanisha viongozi wetu wakubwa wa nchi mbalimbali" Amesema Mhe. Senyamule 

Akisoma risala yake mbele ya mgeni rasmi, Askofu Daniel Kitua wa Kanisa la Talitha Cuni na Mratibu wa Kongamano, Maombi hayo yameleta mafanikio chanja kwa jamii za Afrika.

"Tangu kuanza Maombi haya, tumeshuhudia kuenea kwa Neno na kuhudumia Kiroho na kimwili, Kanisa kuona thamani ya Maombi kwa kuombea nchi na hata kuombeana wenyewe kwa wenyewe, kiu ya Maombi imeongezeka baina ya waumini na Serikali inatoa ushirikiano kwa Taasisi za Kidini pale unapohitajika" Askofu Kitua.

Kongamano hilo, lilianza rasmi 2023 na hili ni la pili mwaka huu, likiongozwa na Neno; "Ni nani atakayesimama kwa ajili yangu juu ya wabaya? Ni nani atakayesaidia juu yao wafanyao maovu?" (Zab. 94:16) na linakutanisha wanamaombi kutoka nchi za Burundi, Congo, Kenya, Zambia, Ubelgiji, Watanzania wanaoshi Ufaransa na wengine kutoka mikoa tofauti tofauti hapa nchini.


#keroyakowajibuwangu
#dodomafahariyawatanzania

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA