WENGE WA UHURU DODOMA KUPITIA MIRADI YENYE THAMANI ZAIDI YA SH.BILIONI 21.2










Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma unatarajiwa kupitia jumla ya miradi 56 yenye thamani ya Jumla  ya Shilingi Bilioni 21.2. Mwenge huo utakimbizwa kwa siku nane katika Halmashauri zote nane za Mkoa huo na utakimbia kwa Kilometa 1,484  .

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 27.06.2024 na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akipokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Mpira wa Kata ya Chipogoro kwenye Wilaya ya Wilaya ya Mpwapwa kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba.

Mhe. Senyamule amesema Mwenge huo utakuwa chachu ya uzinduzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kimkakati kwenye Mkoa wa Dodoma kwa maendeleo ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule ameeleza kuwa kwa sasa Mkoa  huo  unaendelea na uhamasishaji wa wananchi kuhakiki majina yao katika daftari la kudumu la mpiga kura sambamba na kuwahamasisha kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi mkuu wa 2025.

Akizungumzia suala la kiafya amesema kuwa wanaendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima afya zao kwa hiari ili kutambua hali halisi ya usalama wao.

Hata hivyo, ameeleza kuwa hali ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa Mkoa wa Dodoma imeshuka kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia moja ya maambukizi yake.

Kadhalika kwa upande wa  mazingira amesema, Mkoa wa huo  unaendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti ya kutosha ikiwemo miti ya kivuli na matunda jambo ambalo litasaidia Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani.

Mwenge wa Uhuru 2024 unaongozwa na kauli mbiu ya: "tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu"


&&&


#mwengewauhuru2024 
#dodomafahariyawatanzania
#keroyakowajibuwangu

 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA