ASKARI POLISI WA WILAYA YA DODOMA AKABIDHIWA PIKIPIKI







Na Sofia Remmi 
Habari-Dodoma Rs

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar K.Mmuya leo tarehe 28 Oktoba 2024,amekabidhi pikipiki moja kwa askari polisi wa Wilaya ya Dodoma kwa ajili ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma na kufuatilia,kuzuia uhalifu na ukatili utakao jitokeza katika Wilaya hii.

Kifaa hicho kimetolewa na Kituo Jumuishi kwa Manusura wa vitendo vya ukatili wa Kijinsia na ukatili dhidi ya watoto(One Stop Centre) kilichopo katika hospital ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni moja ya jitihada za kutokomeza ukatili wa Kijinsia
Kituo hicho kinajumuisha Maafisa Ustawi wa Jamii,Madaktari,Wauguzi na Polisi,

Huduma zinazotolewa katika kituo hicho jumuishi ni pamoja na kupokea na kushughulikia taarifa zote za ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto,kutoa huduma ya matibabu ikijumuisha uchunguzi wa ukatili aliofanyiwa Manusura,matibabu na majeraha,utoaji wa kinga dhidi ya VVU na uzazi wa mpango wa dharura kwa Manusura,kutoa ushauri nasaha na kuwalinda,kuelimisha jamii kuhusu ukatili,kufuatilia na kupokea taarifa kuhusu kesi za rufaa mbalimbali na kuandaa kutunza na kuwasilisha kumbukumbu au ripoti.

#kurayakosautiyako.
#dodomatupotayarikupigakura
#ujanjanikupigakura
#mtiwangbirthdayyangu.
#Keroyakoaajibwangu 
#dodomafahariyawatanzania






 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA