KAMATI YA BUNGE TAMISEMI YATEMBELEA SOKO LA MACHINGA DODOMA













Na. Hellen M. Minja,
       Habari – DODOMA RS

Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo Oktoba 28, 2024, imefanya ziara ya kikazi katika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na baadae  kukagua soko la wazi laWajasiriamali Wadogo (Machinga) lililojengwa katika kata ya Majengo, Mtaa wa Kitenge, tawi la Bahi Road.

Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Justin L. Nyamoga pamoja na naibu waziri wa TAMISEMI Mhe. Festo Dugange, imetembelea na kujionea namna soko hilo lililojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu pamoja na mapato ya ndani ya Halamashauri ya Jiji la Dodoma linavyoendeshwa.

Akizungumzia ukusanyaji wa ushuru wa soko kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wakati akitoa taarifa ya uendeshaji wa soko hilo la wazi la Machinga, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dkt. Frederick D. Sagamiko amesema;

“kwa kipindi cha Julai, 2023/Juni 2024, soko la Machinga limeweza kukusanya kiasi cha shilingi Milioni 460 kati ya bilioni 1 iliyokisiwa, sawa na 46% ya lengo. Mwaka wa fedha 2024/2025, jumla ya shilingi 1,902,895,000 zimepangwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya soko na kwa kipindi cha robo ya kwanza, shilingi 130,346,801 zimekusanywa” Dkt. Sagamiko

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amesema;

“Nitafuatilia idadi kamili ya watu waliopo pale ili kupata uhakika kamili wa mapato yanayozaliwa. Juhudi mbalimbali zimefanyika ili kufanya uhai wa lile soko uweze kuongezeka kwani kila mwaka tumekua tukifanya kile kinachowezekana ili kufikia mahitaji yote ambayo machinga wamekua wakiyaomba”.

Nae, Katibu wa soko hilo Bw. Marko S. Mwagale, amezungumzia changamoto kadhaa zinazoendelea kulikabili soko hilo huku akitaja uchache wa wateja wanaofika hapo kutokana na idadi ndogo ya mabasi ya abiria wa ndani maarufu kama daladala zinazopakia na kushusha abiria sokoni hapo.

Akihitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ametoa maelekezo kadhaa yakiwemo; kusitishwa kwa zoezi la kutafuta Mzabuni wa soko, kuweka mfumo wa malipo ya ushuru kwa ‘control number’, miundombinu ya eneo la wauza mbogamboga iboreshwe pia, Kamati imehitaji kupatiwa mpango juu ya eneo la Sabasaba lililopo Jijini humu.

 

#kurayakosautiyako               
#ujanjanikupigakura    
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu












 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA