MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHMINI KWA WATUMISHI WA TAMISEMI YAFUNGWA RASMI











Na Sofia Remmi.
      Habari-Dodoma Rs.

Katibu tawala mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya amefunga mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini yanayoendeshwa na chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa watumishi waTawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa leo tarehe 25 Oktoba 2024.

Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya serikali kuhakikisha maofisa hao wanasaidia kukamilisha mipango ya Serikali katika kupeleka shughuli za maendeleo kwa Wananchi kwa kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji pamoja na tathmini ya maendeleo ya miradi inayotekelezwa na Serikali katika maeneo ya mamlaka hizo.

Hii ni awamu ya kwanza kwa mafunzo hayo yaliyoanza Oktoba 21, 2024 na kumalizika leo Oktoba 25,2024,kufanyika katika mkoa huu, yakihusisha maafisa takriban 90 wanaosimamia vitengo vya ufuatiliaji na tathmini katika Halmashauri, Manispaa, Majiji na Mikoa kutoka katika mikoa 15 Nchini.

#kurayakosautiyako
#dodomatupotayarikupigakula
#ujanjanikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu










 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA