MAONESHO YA MAUA YAZINDULIWA CHINANGALI PARK DODOMA









Na. Hellen M. Minja,      
       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amezindua maonesho ya maua Mkoa wa Dodoma Oktoba 25, 2024, yanayowahusisha wanawake wa kikundi cha wanawake wauza maua Mkoani hapa wakishirikiana na wenzao kutoka mikoa ya Arusha, Dar Es Salaam na Kilimanjaro.

Maonesho hayo ya siku tatu ambayo yameanza leo Oktoba 25 hadi Oktoba 27, 2024, katika viwanja vya Chinangali Park, yanalenga kukuza uelewa wa kutunza mazingira kwa kupanda miti na maua huku yakiongozwa na kauli mbiu ya “Panda maua na miti, pendezesha Dodoma”

Akizindua maonesho hayo,Mkuu wa Mkoa, alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wasimamizi wa majengo ya Serikali, kupanda  maua katika majengo hayo ili kupendezesha mandhari, lakini pia kupata hewa safi.

“Nitoe wito kwa ofisi zote za Serikali Mkoa wa Dodoma, majengo yale yawe na oksijeni ya kutosha kwa kupanda maua, yawe na hewa ya kutosha na nzuri kwa kupanda maua, yawe na mvuto wa kutazamika vizuri kwa kupanda maua” Amesema Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K.Mmuya, amesema kuwa Mkoa upo tayari kushirikiana na wajasiriamali hao wa maua kutafuta eneo maalum kwa ajili ya kupanda, kufanyia biashara, pamoja na kutoa elimu juu ya umuhimu wa maua.

Awali, akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mratibu wa maonesho hayo Bi. Suzan Kabogo, amezitaja faida za maua kwenye maisha ya binadamu.

“Maua yana faida katika maisha yetu ikiwa ni pamoja na kutupatia oksijeni, kuboresha afya ya akili kwani kwa kutazama mandhari nzuri ya maua, husaidia kupunguza msongo wa mawazo.                         



#kurayakosautiyako    
#ujanjanikupigakura                
#dodomatukotayarikupigakura
#mtiwangubirthdayyangu








 

Comments

Popular posts from this blog

WALIMU WATAKIWA KUFUNDISHA UZALENDO SHULENI.

TRAMPA KANDA YA KATI WAFANYA KIKAO DODOMA

BARAZA LA MITUME NA MANABII WAMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA