SEKRETARIETI YA MKOA WA DODOMA WAPIGWA MSASA.
Na. Sizah Kangalawe Habari - RS Dodoma
Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huu Bw. Kaspar Mmuya, wamepatiwa mafunzo mbalimbali ya kiuongozi yanayolenga kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Mafunzo hayo yamefanyika Oktoba 26,2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hii, yakiwajumuisha Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa vitengo, ambapo katibu tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar Mmuya ametumia fursa hiyo kuwaagiza Viongozi hao kuyatumia maarifa waliyonayo kwa vitendo zaidi.
"Niwaombeni tuu huko mbele tuendako myatoe maarifa mliyonayo na kuyaweka kwenye vitendo.Na ili mfanye, ni lazima muwe 'systematic' kuendana na miongozo inayotakiwa, maana yake ni kutojitoa ufahamu na kufanya unavyotaka wewe. Ni lazima ufuate muongozo,kwa sababu hicho unachotakiwa kufanya kinabebwa na cheo chako na sio jina lako", amesema Mmuya
Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo Mhadhiri Mwandamizi kutoka chuo Kikuu Huria cha Tanzania Dkt. Emmanuel J. Mallya, amewasihi Viongozi hao kuhakikisha wanakuwa sababu ya kupunguza maumivu na kuongeza furaha kwa Watumishi wanaowaongoza, ili watekeleze majukumu yao kwa weledi unaotakiwa.
Naye mtaalam Mbobezi wa Ufuatiliaji na Tathmin Bw. Richard Ugulumu, ameisihi Menejimenti hiyo kujiwekea utaratibu mzuri wa kufanya tathmin juu ya malengo waliyojiwekea, ili kujua wamefanikiwa kwa kiasi gani katika utekelezaji wa malengo yao.
" Serikali imeweka utaratibu wa
Ufuatiliaji na kufanya tathmin ya utekelezaji wa kazi za kila siku, na lengo la kufanya tathmin ni kujua changamoto ziko wapi na kuchukua tahadhari mapema ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea na yanayotokana na bajeti ya Serikali inayotolewa kwa lengo la kuteleza miradi, na Serikali inatoa Mwongozo wa kufanya tathmin hizo". Amesema Ugulumu
Comments
Post a Comment